The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Zitto Kabwe: Hivi Hapa Vitabu Vyote Nilivyosoma 2024

Mwaka 2024 haukuwa mwaka mzuri sana kwangu binafsi katika usomaji wa vitabu, nikisoma vitabu vichache sana ukilinganisha na miaka mingine iliyotangulia.

subscribe to our newsletter!

Mwaka 2024 haukuwa mwaka mzuri sana kwangu binafsi katika usomaji wa vitabu, nikisoma vitabu vichache sana ukilinganisha na miaka mingine iliyotangulia: 25 mwaka 2023; 33 mwaka 2022; na 29 mwaka 2021. Mwaka huu nimesoma vitabu 17 tu. 

Nilinunua na kupewa zawadi ya vitabu vingi, lakini sikupata muda wa kuvisoma, au kuvisoma na kumaliza.

Baada ya kumaliza muda wangu wa uongozi kwenye chama cha ACT Wazalendo, nilidhani kwamba nitakuwa na muda wa kutosha wa kusoma, kuandika na kupumzika. Haikuwa hivyo hata kidogo. Nilijidanganya. Nilitumia muda mwingi zaidi katika shughuli za chama kuliko miaka yote ya uongozi wangu katika chama.

Ni dhahiri kuwa mwaka 2025 utakuwa mgumu zaidi katika usomaji wa vitabu. Tutaona.

Mwaka huu pia nimesoma shaghala baghala, yaani bila mpangilio. Sikuwa mandhari, au theme, kwa kimombo, maalumu. Ingawa kuna vitabu vichache vina mandhari ya kupigania demokrasia, inaweza kudhaniwa nilipangilia. Hapana, imetokea tu.

Miaka ya nyuma mtu akitazama orodha yangu anaweza kueleza kwa ufasaha nchi nilizotembelea, au hata mawazo yaliyokuwa kichwani mwangu muda mwingi wa mwaka. Si kwa mwaka 2024. Sababu kadhaa zinaeleza hilo. 

SOMA ZAIDI: Viongozi Hawa Kumi wa Tanzania Watakuhamasisha Kupenda Kusoma Vitabu

Kwanza, sikusafiri sana nje ya nchi, ukiacha safari chache za kikazi katika ukanda wa SADC na Afrika Mashariki ambapo ni safari za kuingia na kutoka bila kupata muda wa kutosha wa kutembelea maduka ya vitabu. Pili, ni kama nilikuwa nasoma bila mpangilio haswa wa nini nataka kwa kweli, na hivyo kukosa theme maalumu.

Mwaka huu wa 2024 pia nimesoma riwaya chache sana kulinganisha na miaka ya nyuma.

Kitabu changu cha kwanza kusoma na kukimaliza katika mwaka – China Economic Miracles: Does FDI Matter? cha mwandishi Sumei Tang na wengine – kilitokana na hitaji la kufanya mhadhara wa uchambuzi wa kitabu, ombi kutoka Taasisi ya Uongozi. 

Kitabu changu cha mwisho – How to Stand Up to a Dictator: The Fight for our Future cha mwandishi Maria Ressa – ni zawadi kutoka kwa mwanangu, Wiza-Chachage. Ni kitabu kizuri sana kiasi nimemshauri mmoja wa wadogo zangu ambaye ni Mhariri wa chombo cha habari akisome.

Hata hivyo, nimesoma, na nina hamu ya kukushirikisha kwenye vitabu vichache nilivyofanikiwa kuvisoma kwa mwaka huu wa 2024. Vifuatavyo ni vitabu hivyo:

  1. China’s Economic Miracles: Does FDI Matter? – Sumei Tang, Eliyathamby A. Selvanathan & Saroja Selvanathan.
  2. Nigeria’s Soldiers of Fortune: The Abacha and Obasanjo Years – Max Siollun.
  3. Wivu Bustani ya Edeni – Dotto Rangimoto.
  4. And Home was Kariakoo: A Memoir of East Africa – M. G. Vassanji.
  5. The Wizard of the Kremlin – Giuliano Da Empoli.
  6. Politics On the Edge – Rory Stewart.
  7. Rich State, Poor State – Greg Mills.
  8. Accelerating India’s Development – Karthik Muralidharan.
  9. Inside The War Room – Ma Trong Tham.
  10. Sokoine: Maisha na Uongozi wake – Uongozi Institute & Sokione University.
  11. The Abiy Project: God, Power and War in the New Ethiopia – Tom Gardner.
  12. The Park Chung Hee Era: The Transformation of South Korea – Byung-Kook Kim & Ezra F. Vogel.
  13. The History of Ideas – David Runciman.
  14. The Road to Freedom: Economics and the Good Society – Joseph Stiglitz.
  15. How Tyrants Fall and How Nations Survive – Marcel Dirsus.
  16. Defeating The Dictators: How Democracy Can Prevail In The Age of The Strongman – Charles Dunst.
  17. How To Stand Up To A Dictator: The Fight for Our Future – Maria Ressa.

Nawatakia kheri katika mwaka 2025, mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Kwa hakika, kama nilivyotangulia kusema, mwaka huu utakuwa na heka heka nyingi. 

Kwa uwezo wake Mola tutauvuka salama na HAKI itatamalaki katika taifa letu!

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

7 responses

  1. Assalamu aleykum wallahamtullah kiongozi samahani kwa usumbufu ila nakuomba msaada wako nimekwama ada ya kumalizia chuo katka kozi ya ualimu chuo kikuu Cha sokoine

    Mawasiliano yangu 0743430388 pia 0787549515

  2. Habari Mh. Z. KABWE, naombaunisaidie mambo mawili tu.
    1. Nawezaje kupata VITABU Kwa gharama nafuu? (Kwenye mtandao na maanisha)
    2. Kusoma ni kazi inahitaji Moyo (UNATUMIA mbinu Gani kufanikiwa)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts