The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Polisi Watoa Taarifa Kuhusu Tukio la Kupotea Kwa Danstan Daud Mtajura. Danstan Anafahamika Kwa Kazi Zake Kama Afisa Mwandamizi Serikalini

Danstan Daud Mtajura ni Afisa Mwandamizi wa serikali aliyehusika katika majadiliano mbalimbali katika sekta ya madini

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wametoa taarifa ya kufuatilia tukio la kupotea kwa Danstan Daud Mtajura, hii ni baada ya kusambaa kwa taarifa za kutekwa kwake mnamo Januari 04, 2025.

“Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Januari 04,2025, majira ya saa 8 mchana ilipokea taarifa kutoka kwa wananchi ya kuonekana kwa gari aina ya Mercedes Benz T109 DVY iliyokuwa imetelekezwa eneo la Buza Sigara. Taratibu zilifanyika na gari hilo likavutwa hadi kituo cha Polisi Buza,”inaeleza taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Januari 05,2025.

Tarifa hiyo inaendelea: “Tarehe 05 Januari 2025, katika kituo cha Polisi Chang’ombe zimepokelewa taarifa kutoka kwa ndugu kuwa gari hiyo iliyotelekezwa ilikuwa inaendeshwa na ndugu yao aitwaye Dastan Daud Mtajura,” taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa toka Januari 04, 2025, Danstan hakuonekana toka alivyotoka nyumbani kwake. Polisi wameeleza kuwa bado wanaendelea na ufuatiliaji wa tukio hilo.

Danstan anafahamika zaidi kwa kazi zake kama Afisa Mwandamizi serikalini, ambapo mnamo Julai 18, 2022, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi mwakilishi wa serikali atakayesimamia hisa za serikali katika kampuni ya uchimbaji madini Kinywe (Graphite) ya Faru Graphite, ambayo imeundwa na Black Rock Mining ya Australia (84%) na Serikali ya Tanzania (16%). Kampuni hiyo inafanya uchimbaji wa madini Kinywe katika eneo la Mahenge, eneo linalojulikana kuwa la pili duniani kwa wingi wa madini kinywe yaliyopo ardhini.

Katika taarifa iliyotolewa na kampuni ya Black Rock kuhusu uteuzi wa Danstan mnamo Julai 2022, inaeleza kuwa alikuwa akifanya kazi kama mtaalamu wa madini, mshauri na mratibu wa timu za majadiliano ya kimkakati katika sekta ya madini ikiwemo, timu maalum ya majadiliano katika ofisi ya Rais.Taarifa mbambali zinaonesha pia Danstan amewahi kufanya kazi kama mkaguzi katika viwanja vya ndege nchini.

Taarifa za kupotea kwa Danstan zilianza kusambaa mnamo Januari 04, 2025, kupitia ujumbe katika mitandao ya kijamii.

“Danstan ametekwa leo majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Sigara, TANESCO, Buza,” taarifa hiyo iliyoanza kusambaa usiku ilieleza. “Madereva wa bodaboda walioshuhudia tukio hilo wamesema Danstan alinyofolewa kutoka kwenye gari lake na kufungwa kitambaa usoni huku akilalamika kuwa alikuwa akitekwa,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Danstan alitekwa na watu waliokuwa na silaha za moto wakiwa katika gari jeupe, jalada la shauri hilo limefunguliwa kwa namba ya rejea, RB No.BZA/RB/53/2025, katika kituo cha Polisi cha Buza.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts