The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Tunawaandaje Mabinti Zetu kwa Ajili ya Hedhi Yao ya Kwanza?

Familia zetu zinapoongea kwa uwazi na bila kejeli kuhusu hedhi, tunavunja ukimya na unyanyapaa unaozunguka afya ya uzazi katika jamii zetu.

subscribe to our newsletter!

Kuna siku katika maisha yetu wazazi ambayo hubeba hisia nyingi, na ni siku ambayo binti yetu anapata hedhi yake ya kwanza. Ni siku inayoweza kuja ghafla, ikibeba mshangao, furaha na hata hofu kidogo. Kwa binti, ni ishara ya ukuaji; kwa sisi wazazi, ni ukumbusho kwamba mtoto wetu anaanza safari mpya ya kuelekea utu uzima.

Ni jambo la kawaida, lakini limekuwa likizungukwa na ukimya, aibu, au hofu. Mara nyingi huwa tunasubiri hadi binti anapokaribia kupata hedhi ndipo tuzungumze, lakini ukweli ni kwamba kadiri tunavyowahi kuwaelimisha na kuwaandaa kwa ajili ya siku hiyo, ndivyo tunavyomjengea ujasiri. 

Wazazi tunajukumu la kuhakikisha kwamba mabinti zetu wanalipokea kama sehemu ya kawaida ya maisha yao, si kama kitu kinachotisha.

Hii huanzia nyumbani, kuzungumza nao mapema, kwa uwazi na upole, ili kuawaondolea wasiwasi. Tuwaeleze kiundani kuhusu mabadiliko yanayotokea katika mwili wa mwanamke pale wanapobalehe (puberty) na kwamba hedhi si ugonjwa bali ni ishara ya ukuaji wa kawaida. Kwa kufanya hivyo, tunawajengea hali ya kujiamini na utulivu wa hisia.

Kwenye jambo hili, wazazi wote wawili tuna nafasi muhimu. Mama anaweza kumfundisha binti jinsi ya kutumia taulo za kike (pedi), namna ya kubeba pedi chache kwenye begi lake la shule, na pia kumfundisha jinsi ya kuufahamu mzunguko wake na hata kuuandika kwenye daftari au simu. 

SOMA ZAIDI: Kwa Nini ni Umuhimu kwa Watoto Kuwatembelea Bibi na Babu Zao?

Kwa njia hii tunawasaidia wawe tayari, hata kama hedhi itawakuta wakiwa darasani au mbali na nyumbani.  Tunaweza pia kuwaelezea stori ya ilivyokua siis tulivyopata hedhi yetu ya kwanza.

Akina baba na sisi tuna wajibu. Mara nyingi baba huachwa kando kwenye mazungumzo haya, lakini tunaposimama katika nafasi yetu kama mzazi kwa utulivu na uelewa, tunavunja ukuta wa ukimya. 

Tunaweza kuzungumza na binti zetu kwa upole kuwaeleza kuwa kupata hedhi si kitu cha aibu, bali ni sehemu ya ukuaji wake. Pia, tunaweza kuhakikisha binti zetu wanapata mahitaji muhimu kama taulo za kike (pedi) shuleni na nyumbani na kwa njia hiyo kumjengea hisia kwamba hana haja ya kuficha au kuona aibu. 

Hata maneno ya kawaida kama, “Usijali, uko sawa, kila kitu kiko sawa,” yanaweza kumpa binti nguvu kubwa ya kujiamini.

Iwapo hedhi ya kwanza itatokea shuleni, binti aliyeandaliwa mapema hataingiwa na hofu. Atajua cha kufanya, kubadilisha nguo za ndani na kutumia taulo aliyobeba, au kuomba msaada kutoka kwa mwalimu au rafiki anayemwamini. Huu ndiyo ujuzi na nguvu tunayowapa watoto wetu kupitia maandalizi na mazungumzo ya mapema.

SOMA ZAIDI: Tujifunze Tunavyoweza Kuwasaidia Watoto Wetu Kwenye Safari Yao ya Elimu

Zaidi ya yote, tunaposhirikiana kama wazazi, tunawajengea mabinti picha thabiti kwamba hedhi ni jambo la kawaida. Familia zetu zinapoongea kwa uwazi na bila kejeli kuhusu hedhi, tunavunja ukimya na unyanyapaa unaozunguka afya ya uzazi katika jamii zetu na kuwafundisha kwamba wanathaminiwa katika kila hatua ya maisha yao. 

Makala hizi za malezi huandaliwa na C-Sema, shirika lisilo la kiserikali linalojikita katika kuendeleza na kulinda haki za watoto Tanzania. Kwa maoni na ushauri, wapigie kwenye simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile, unaweza kuwapata kupitia kurasa za Facebook: Sema Tanzania, X: @SemaTanzania, na kupitia tovuti yao www.sematanzania.org.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×