The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Filamu Yaonesha Haikua Kazi Ngumu kwa Polisi Tanzania Kumkamata Mhalifu Aliyetoroka Jela Afrika Kusini, Thabo Bester na Mpenzi Wake Dk. Nandipha Baada Kazi Hiyo Kushindikana Afrika Kusini

Kachero wa Tanzania aliyehojiwa katika filamu hiyo alieleza ukamataji ulikuwa rahisi kama kumkamata kuku

subscribe to our newsletter!

Ilichukua maneno 53 pekee kwa Polisi Tanzania kuelezea katika ripoti waliyotoa Aprili 08, 2023, juu ya kumkamata Thabo Bester, mhalifu aliyetoroka gerezani Afrika Kusini akisaidiwa na mpenzi wake Dk. Nandipha Magudumana. Ilikuwa ni habari kubwa iliyotikisa Afrika Kusini, Afrika kwa ujumla na duniani, maneno 53 ya Polisi Tanzania, hayakukata kiu ya wengi waliotaka kuelewa ilikuwaje na walikamatwaje.

Habari hii imeendelea kushika kasi hata sasa ambapo hukumu ya wawili hao hasa Dk. Nandipha ikisubiriwa,kwani Bester amesharudi gerezani kuendelea na kifungo chake cha maisha. Katika kukata kiu hii ya wafuatiliaji wengi, Ijumaa ya Septemba 12, 2025, mtandao wa Netflix umeachia filamu yenye sehemu tatu yenye jina la Beauty and the Bester.

Filamu hiyo imeangalia tukio zima: kuanzia lilivyosukwa mpaka Bester kuweza kutoroka gerezani, kuishi kifahari uraiani na kuendesha biashara kadha wa kadha, pamoja na uzoefu kutoka kwa makachero, waandishi wa habari, na familia za Bester na Dk. Nandipa. Bester na mwenzake walienda Mahakamani kujaribu kuzuia filamu hiyo, hata hivyo hawakufanikiwa kumashawishi Jaji Sulet Potterill wa Mahakama Kuu ya Afrika Kusini.

Kipande cha mwisho cha filamu hiyo kinaeleza namna Bester na Nadhipha walivyoweza kukamatwa Tanzania, ambapo kachero wa Tanzania ambaye hakutambulishwa alieleza ukamataji ulikuwa rahisi kama kumkamata kuku.

Gari lao liliweza kusimamishwa na makachero waliokuwa wakiwafuatilia wakiwa wanajaribu kuvuka mpaka wa Tanzania na Kenya. Ukamataji huu ulikuja baada ya kazi hiyo kushindikana Afrika Kusini, toka ambapo Polisi wa nchi hiyo waanze kuwasaka katika maeneo mbalimbali nchini humo mnamo Machi 2023. Katika taarifa ya polisi Tanzania waliyoitoa Aprili 08, 2023, walieleza watuhumiwa hao walikamatwa pamoja na mtu mmoja ambaye ilikuja kufahamika kuwa alikuwa ni raia wa Msumbiji.

“Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kutoa ufafanuzi baada ya watu mbalimbali kuuliza kuhusu taarifa za kukamatwa Raia wa Afrika Kusini hapa nchini,”ilieleza taarifa ya Polisi Tanzania ya Aprili 08, 2023.

“Ni kweli makachero wetu wamewakamata Thabo Bester, Dr. Nandipha Magudumana na Zakaria Alberto na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Taratibu za mawasiliano ya kisheria ya ndani na ya kimataifa zinaendelea kukamilishwa,” iliongeza taarifa hiyo.

Kabla ya kutoroka jela, Thabo Bester alikuwa akitumia kifungo cha maisha gerezani toka mwaka 2012, katika gereza la Mangaung la Afrika Kusini, kwa makosa ya ubakaji na mauaji. Hata hivyo ilithibitika kuwa ametoroka gerezani baada ya gazeti la uchunguzi la Ground Up, kuchapisha picha zake akijivinjari katika maduka ya nguo pamoja na Dk. Nandipha.

Taarifa rasmi za gerezani ni kuwa Bester alifariki gerezani kwa kujichoma moto mnamo Mei 2022, hata hivyo ilikuja kuthibitishwa kuwa haikuwa hivyo, na mpenzi wake Dk. Nandipha ndiye aliyetafuta mwili wa wa mtu mwingine uliotumika kumwezesha kutoroka jela.

Chumba cha gereza ambacho Bester alikua akikaa kilishika moto mnamo Mei 3, 2022, na uliokuwa ukidaiwa kuwa mwili wake uliungua kabisa. Hata hivyo ilikuja kugundulika baadae mwili huo haukuwa wa kwake, ni mwili uliotafutwa na Dk.Nandipha ili kutumika kama geresha tu.

Pamoja na uwepo wa mashaka kuhusu kifo cha Bester, alifanikiwa kuishi kifahari Afrika Kusini, ikiwemo kuanzisha biashara mbalimbali akiwa pamoja na mpenzi wake. Hata hivyo habari ya Bester na Dk. Nandipha ilibadilika kabisa mnamo Machi 2023,pale ambapo picha ya Bester na Nandipha wakinunua mavazi pamoja ilivyochapishwa.

Habari ya Nandipha na Bester imeendelea kuwaacha watu katika maswali mengi hasa kwa kuwa Nadnipha alikuwa mwanamama maarufu Afrika Kusini, Daktari aliyekuwa akimiliki taasisi ya mamilioni, huku mahusiano yake na Bester yakianza wakati Bester akiwa tayari gerezani.

Baada ya kukamatwa Tanzania, Nandipha na Bester walikabidhiwa kwa ubalozi wa Afrika Kusini, walioweza kuwarudisha Afrika Kusini kwa ndege binafsi mnamo Aprili 12, 2023, ambapo kesi yao ilifunguliwa rasmi, huku wote wakirudishwa gerezani, Nandipha akiwa rumande, na Bester akiendelea kutumikia kifungo chake cha maisha.

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×