The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search Results for: muungano – Page 15

Ismail Jussa: Sikubaliani na Hoja Kwamba Mchakato wa Katiba Mpya Uanze Baada ya 2025

Mjumbe huyo wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar anasema mchakato wa kudai Katiba Mpya unaweza kwenda sambamba na ule wa kudai mageuzi madogo kwenye mfumo wa usimamizi wa uchaguzi nchini, na kwamba si suala la kipi kitangulie kipi, huku akidai hiki ndiyo chama chake cha ACT-Wazalendo kinachomaanisha kwa kauli mbiu yake ya Tume Huru Kuelekea Katiba Mpya.

Mwaka Mmoja Bila Magufuli: Alipotuacha Na Anapotupeleka Rais Samia

Katika makala hii, Mbunge wa Ubungo (CCM) Profesa Kitila Mkumbo anarejea mchango wa Rais Magufuli katika ujenzi wa Tanzania kwa kuainisha pale Magufuli alipoikuta Tanzania na alipoiacha wakati anafariki, na hivyo kujenga msingi wa kuelewa Tanzania inapoelekea chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Wanasiasa, Wanaharakati Wataka Masheha Wapigiwe Kura Zanzibar

Kumekuwapo na tuhuma kwamba katika utekelezaji wa majukumu yao Masheha wamekuwa wakikipendelea chama cha CCM na wakila njama za kuvidumaza vyama vya upinzani. Tuhuma hizi huibuka zaidi wakati wa michakato ya chaguzi kuu kuanzia utoaji wa kadi za Mzanzibari Mkaazi na usajili wa daftari la wapiga kura.

Changamoto za Upatikanaji Vifaa Yakwamisha Kukamilika Kwa Mradi wa Fedha za Tozo

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kata ya Idetemya iliyopo Misungwi mkoani Mwanza ilitegemewa kukamilika Januari 10,2022, lakini kutokana na changamoto za upatikanaji wa vifaa vya ujenzi mradi huo utakamilika Februari 28,2022. Mradi huo unagharimikiwa na fedha za tozo ya miamala ya simu

×