The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Hizi Hapa Habari Kubwa Zilizochapwa Kwenye Kurasa za The Chanzo 2023

Ni habari zilizopigiwa kura na waandishi wa habari wenyewe wa The Chanzo.

subscribe to our newsletter!

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki saa chache ili tuumalize mwaka huu wa 2023. Mwaka ambao The Chanzo imeendelea kuchapisha habari zinazolenga kuwawezesha Watanzania kuielewa nchi yao na yanayotokea ili wawe na nafasi nzuri zaidi ya kufanya maamuzi juu ya hatma ya jamii na taifa lao kwa ujumla.

Waandishi weledi na mahiri wa chombo hiki cha habari waliosambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi – Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Mtwara na Zanzibar – wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii kuwapatia Watanzania maana zilizojificha nyuma ya vichwa vya habari.

Tunakuwekea hapa orodha ya habari 10 kubwa na bora zilizochapishwa na The Chanzo kwa mwaka huu, habari ambazo zimechaguliwa na kupigiwa kura na waandishi wa habari wenyewe:

Na hii ndiyo orodha ya habari hizo; 

Undani Kuhusu Mtanzania Aliyefariki Nchini Ukraine. Familia Yazungumza 

Habari hii ilikuwa inamhusu Mtanzania Nemes Tarimo aliyeuawa Oktoba 24, 2022 katika mji wa Bakhmut huko nchini Ukraine wakati akipigana vita vinavyoendelea akiwa upande wa Urusi chini ya vikosi vya kampuni binafsi ya ulinzi ya Wegner. 

Mara baada ya kupokea taarifa za kifo cha ndugu yao familia yake ilikuwa katika harakati za kuwasiliana na Serikali ili kuweza kuurudisha mwili wa marehemu nchini kwa ajili ya mazishi. Kitu ambacho baadaye walifanikiwa

The Chanzo ilifanya uchunguzi wake na kueleza safari nzima ya Tarimo kwenda Urusi, kukamatwa, kufungwa na hadi kujikuta akiingia vitani.

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Askari wa Hifadhi Kilwa Wadaiwa Kukiuka Haki za Binadamu Wakiwahamisha Wananchi Kwenye Ardhi Yenye Mgogoro 

Hii ni habari iliyofanywa na mwandishi wa The Chanzo kutoka Mtwara Omari Mikoma, ikihusu wananchi wa kijiji cha Mtepera, wilayani Kilwa, mkoani Lindi ambao walikuwa wakidai kunyanyaswa na askari wa hifadhi kwa lengo la kuwashinikiza kuondoka kwenye ardhi yenye mgogoro. 

Kijiji hicho kinachopakana na Hifadhi ya Wanyamapori ya Selous kinakadiriwa kuwa na wakazi 2,000 ambayo walikuwa kwenye mvutano na hifadhi hiyo iliyodaiwa kumega takribani ekari 18,000 na kuzijumuisha kwenye eneo la hifadhi. 

Kitendo hicho kilipelekea kaya zipatazo 150 kukosa makazi baada ya kulazimishwa kuhama kwenye eneo hilo. 

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Should Banks Manage 10pc Local Government Loans?

Serikali ya Tanzania ilisitisha utolewaji wa mikopo iliyokuwa ikitolewa na halmashauri nchini kwa makundi maalum ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kufuatia Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2021/22 kubaini ubadhirifu mkubwa.

The Chanzo kupitia mtandao wake wa waandishi wa habari nchi iliweza kuwahoji wadau mbalimbali juu ya namna bora ambayo Serikali inaweza itumia kufanikisha utolewaji wa mikopo hii iliyolenga kuwawezesha makundi maalum yaliyoainishwa.

Katika utafiti wake, The Chanzo ilibaini kuwa wadau wengi hususani Asasi za Kiraia, watendaji na wawakilishi wa wananchi kwenye ngazi za Serikali za mitaa wanaona endapo mikopo hiyo itatolewa kupitia mabenki ya kibiashara, lengo la mikopo hiyo litashindwa kufikiwa.

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Meet Brave Zanzibari Men And Women Taking On Child Sex Trafficking: ‘We’ve Got Children Too’

Habari hii ilifanywa na mwandishi wa The Chanzo huko Zanzibar Najjat Omar ikiangazia mtandao ambao ulikuwa ukijishughulisha na vitendo vya kuwaingilia kinyume na maumbile watoto wa kiume huku wakirekodi video na kisha kumfanyia udalali muathirika. 

Vitendo hivyo vilikuwa vikifanywa na wahalifu hao kwa kujifanya wasamaria wema kwa watoto nyakati za usiku, kisha kuwachukua na kuwapeleka nyumbani zao wakiwaahidi kuwapa chakula na malazi kabla ya kuwaingilia. 

Baada ya The Chanzo kuripoti habari hii Jeshi la Polisi Zanzibar liliwakamata watuhumiwa 13 ambao walikuwa wanadaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya udhalilishaji.

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Hanang Disaster: Survival Stories, ‘I thought the floods had affected the entire world’ 

Mwandishi wa The Chanzo kutoka Dodoma Jackline Kuwanda, alifunga safari hadi wilaya ya Hanang iliyopo mkoani Manyara kwa ajili ya kuifanyia kazi habari hii iliyokuwa inaangazia sauti za waathirika wa maporomoko ya tope yaliyowakumba. 

Disemba 3, 2023 wilaya ya Hanang ilikumbwa na maafa hayo yaliyopelekea uharibifu wa nyumba, biashara, miundombinu, majeruhi pamoja na vifo. 

Uzoefu wa siku ya tukio, madhara, na vilio vya wakazi wa Hanang ni baadhi ya mambo ambayo habari hii iliviangazia kwa kiasi kikubwa. 

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Sheria Zinavyokiukwa Zanzibar kwa Kisingizio cha Kuvutia Wawekezaji: ‘Uholela Umetamalaki’

Habari hii iliangazia madai Serikali ya Zanzibar kukiuka Sheria ya Manunuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma, Namba 11 ya mwaka 2016 kwenye utaoaji wa zabuni mbalimbali za Serikali. 

Kitendo hicho kilikuwa ni kinyume na sheria za Zanzibar kwani Serikali inatakiwa kutoa zabuni katika mazingira ya ushindani ili kupata muwekezaji sahihi jambo ambalo lilidaiwa kutofanyika. 

Hali hiyo iliwafanya wadau mbalimbali kuonesha wasiwasi wao kwani uwekezaji mwingi ambao Rais Dk Hussein Mwinyi alikuwa akiupigia chapuo ulionekana kufanyika katika mazingira hayo yanayotishia ustawi wa wananchi na utawala wa sheria. 

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Man, 38, Accuses Police of Torture, Humiliation: ‘I Didn’t Deserve Such Treatments’ 

Habari hii ilikuwa inamhusu Karamba Ramadhani Mnenge, baba wa mtoto mmoja na mkazi wa mtaa wa National Housing jijini Dodoma. 

Mnenge,38, alikuwa analalamikia vitendo vya udhalilishaji alivyodai kufanyiwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kukamatwa akituhumiwa kuvunja na kuiba duka la jirani yake. 

Mara baada ya kufikishwa kwenye kituo cha polisi Dodoma alikaa kwa muda wa siku tatu huku akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kabla ya ndugu zake kufanikiwa kumtoa kwa dhamana. 

Baada ya The Chanzo kuripoti habari hii Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kuwa linachunguza madai ya askari wake kuhusika na vitendo vya ukatili kwa mtuhumiwa huyo. 

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

‘Kila Kukicha Nalia, Sina cha Kufanya’: Waathirika Vitendo vya Ukatili wa Polisi Wataka Uwajibikaji

Habari hii ilifanywa na mwandishi wa The Chanzo jijini Dar es Salaam Lukelo Francis, ikiangazia namna operesheni ya Jeshi la Polisi ya kupambana na kundi la uhalifu linalojulikana kama ‘Panya Road’ ilivyoacha vilio na simanzi kwa baadhi ya familia. 

Hiyo ilitokana na baadhi ya vijana wao kuchukuliwa na Jeshi la Polisi wakiwa nyumbani kwao wakidaiwa kuhusika na kundi hilo, kisha miili yao kupatikana kwenye mochuari ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa na majeraha ya risasi. 

Wadau mbalimbali wakapaza sauti zao wakitaka Jeshi la Polisi kutengeneza mazingira ya kuwajibisha askari wanaotuhumiwa kukiuka maadili ya kazi zao. 

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Simulizi za Wapiga Debe Wanawake Stendi ya Magufuli: ‘Sisi Siyo Mateja’ 

Habari hii ilifanywa na mwandishi wa kujitegemea kutoka Dar es Salaam Anthony Rwekaza ikiangazia jinsi wanawake waofanya shughuli za kupiga debe katika stendi ya mabasi ya Magufuli wanavyofanya shughuli zao. 

Kwa kiasi kikubwa jamii ya Watanzania ina mtazamo hasi dhidi ya kazi hii ya kupiga debe. Hivyo mwandishi alizungumza na baadhi ya wanawake wanaofanya kazi hiyo na kupata simulizi zao jinsi wanavyopata kipato na kusaidia familia zao. 

Habari hii iliibua tatizo kubwa linalowasumbua wanawake wengi nchini ambalo ni suala la rushwa ya ngono. Licha ya kazi hii kuonekana haina taswira nzuri lakini ili kuipata katika eneo hilo rushwa ya ngono ilibainishwa kutamalaki. 

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

‘Sipendi Lakini Inanilazimu’: Simulizi za Wanawake Wanaolea Watoto Masokoni

Habari hii ilikuwa inaangazia mazingira wanayolelea watoto akinamama ambao wanafanya biashara katika baadhi ya masoko jijini Dar es Salaam. 

Uchunguzi wa The Chanzo ulibaini kuwa kina mama wengi wanalazinika kulea watoto wao kwenye mazingira ya soko kutokana na ugumu wa maisha. 

Hata hivyo mazingira hayo yalibainishwa kutokuwa salama kwa malezi kutokana na kutokuwa na kutokuwa na miundombinu rafiki hali ambayo inaathiri ukuaji wa watoto kwa kiasi kikubwa. 

Unaweza kuisoma habari hiyo hapa

Lukelo Francis ni mwandishi wa The Chanzo kutoka Dar es Salaam. Anapatikana kupitia lukelo@thechanzo.com

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts