The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Kitendawili Utekelezaji Dira 2050: Rais Samia Atoa Wito Kuchapa Kazi na Kuacha Mazoea

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dodoma, Julai 17, 2025 amesema ni wakati sasa wa kubadili mtizamo wa namna tunavyofanya kazi na kupimana.

subscribe to our newsletter!

Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 huku akibainisha kuwa ingawa mipango ya dira hiyo imeandikwa na kuandaliwa, mtihani mkubwa utakuwa katika utekelezaji wake.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dodoma, Julai 17, 2025 amesema ni wakati sasa wa kubadili mtizamo wa namna tunavyofanya kazi na kupimana kwani Dira 2050 imeweka shabaha kubwa ya kufikia pato la taifa la Dola za Marekani Trilioni moja.

“Ni wazi kuwa hatutaweza kufikia lengo hili kama tutaendelea kufanya kazi kwa mazoea lazima tubadilike kifikra, kimtazamo na kimatendo, amesema Rais Samia, “Vilevile lazima tupimane kwa matokeo ya kazi.”

Ameiagiza Tume ya Mipango pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha kuwa mchakato wa kuandaa mpango wa maendeleo wa muda mrefu unakamilika kabla ya kuanza kufanya utekelezaji wa Dira 2050 hapo mwakani. 

Dira 2050 imebainisha vigezo mahususi vya kuchagua sekta za vipaumbele, vigezo hivyo ni uwezo wa kuzalisha ajira kwa wingi, uwezo wa kuongeza mauzo nje, uwezo wa kuchochea ukuaji wa sekta nyingine, uwezo wa kuongeza thamani ya mazao yetu hapa ndani na uwezo wa kukuza mapato ya Serikali.

Sekta za kimageuzi tisa zilizochaguliwa kwa sasa ni pamomja na kilimo, utalii, viwanda, ujenzi, madini, uchumi wa buluu, michezo na ubunifu, huduma za kifedha na sekta ya huduma,” amesema Rais Samia.

SOMA ZAIDI: Profesa Shivji: Dira ya Taifa Haina Muda Maalum.Tusikubali Kufanyiwa Majaribio

Amesema pamoja na vigezo hivyo, thamani ya kweli ya Dira 2050 itapimwa kwenye uwezo wa kuitafsiri kwa vitendo katika mipango bajeti na maamuzi mbalimbali.

“Kwa hiyo hatuna budi kuangalia suala la uwajibikaji wa pamoja,” ameendelea, ““Lazima tubadilike kifikra, kimtazamo na kimatendo,” 

Rais Samia anakuwa Rais wa pili kuzindua dira hiyo, baada ya hayati Benjamin William Mkapa kuzindua Dira ya Taifa ya 2025 mnamo mwaka 2000.

Utekelezaji wa Dira 2050 utaanza Julai 2026 baada ya kuisha kwa muda wa dira iliyopo sasa ambayo ni Dira 2025 mnamo Juni 2026.

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango kwa upande wake amesema nchi zote zilizofanikiwa kimaendeleo zilifanya mambo matat;  ikiwemo kuandaa dira za muda mrefu, kuanzisha taasisi za kutafsiri dira na kufuatulia utekelezaji wake.

“Mheshimiwa Rais Dira ya Taifa ni muhimu sana. kwa sababu ndiyo inatupatia ufahamu wa uelekeo lakini pia azma ya taifa. Na inatuwezesha kuunganisha nguvu za raia kuelekea kwenye malengo pamoja na matamanio.”

Dkt Mpango ambaye kitaaluma ni mchami mbobevu amesema kuwa Dira ni muhimu kwa kuwa inachochea matumaini ya wananchi, kuhamasisha wananchi kuchukua hatua, kuongoza maamuzi ya kisera.

“Ningependa kusema kwa nchi kama ya kwetu vijana ndiyo rasilimali yenye nguvu kushinda rasilimali nyingine zote. Na ni muhimu sana tuwekeze juu elimu hii ya dira yetu mpya, Dira ya 2050 kwa vijana ili tuweze kuamsha fikra bunifu za vijana wetu wa kitanzania na kufanikisha utekelezaji wa dira.”

SOMA ZAIDI: Tanzania Inahitaji Dira Moja ya Taifa, Ilani Tofauti za Vyama vya Siasa

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema, dira hiyo, inakuwa dira ya pili ambayo haina muelekeo wa kiitikadi yoyote ya chama cha siasa.

“Huko nyuma na kabla ya kuwa na Dira ya 2025 hakukuwa na mpango wa maendeleo ulioitwa Dira,” amesema Profesa Mkumbo, “Hii haimaanishi kwamba nchi yetu ilikuwa inaongozwa bila Dira ya Maendeleo la hasha kwa hakika tulikuwa na dira katika mipango yetu ya maendeleo.”

“Kwa mfano azimio la Arusha la mwaka 1967  ilikuwa Dira kamili ya nchi yetu ambayo iliongoza mipango ya maendeleo ya nchi kwa miongo mitatu,” ameseieitiza Profesa Mkumbo.

“Hivyo basi wewe mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unakuwa kiongozi wa pili wa nchi yetu kuongoza uandishi wa dira ya taifa wa maendeleo ya miaka 25 kama inavyojulikana leo.”

Jackline Kuwanda ni mwandishi wa habari wa The Chanzo anapatikana mkoani Dodoma: Unaweza kumpata kupitia jaquelinevictor88@gmail.com

Journalism in its raw form.

The Chanzo is supported by readers like you.

Support The Chanzo and get access to our amazing features.
Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Did you enjoy this article? Consider supporting us

The Chanzo is supported by readers like you.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

×
×