
CCM Yakamilisha kura za Maoni ya Uchaguzi Viti Maalum Makundi Mbalimbali, Kivumbi Majimboni Leo
Katika mchakato huu imeshuhudiwa wabunge wawili wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakibwaga na wajumbe kwenye kura zilizopigwa.

Katika mchakato huu imeshuhudiwa wabunge wawili wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakibwaga na wajumbe kwenye kura zilizopigwa.

Katika kipindi cha msamaha, wamiliki wa magari husika watawajibika kulipa kiasi cha ushuru na kodi husika, adhabu na riba vitasamehewa

Makamba amekanusha madai hayo alipoulizwa na waandishi wa habari waliopiga kambi ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutaka kupata maoni yake baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM(NEC) Taifa, kilichoketi Julai 28, 2025 kutomteua kwenye kinyang’anyiro cha ubunge ndani ya CCM jimboni kwake Bumbuli, wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Wabunge zaidi ya 40 ambao wako Bungeni kwa sasa hawataonekana katika kura za maoni ya chama hicho, baadhi ya majina yaliyokumbwa na panga hilo yameendelea kuzua gumzo kubwa mitandaoni.

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa(NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ametoa orodha ya majina ya wana CCM waliopita kwenye mchujo wa Kamati Kuu kwa ajili ya kwenda kupigiwa kura za maoni majimboni kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge na uwakilishhi wa chama hiko kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akitangaza majina ya wanachama wa CCM waliopita katika chujio la Kamati Kuu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla amewataja wananchama wa CCM 11 waliotoka kundi la wabunge 19 waliopita kwenye mchujo wa ubunge wa majimbo na wawili wamepita kwenye mchujo wa ubunge wa viti maalum ngazi ya mkoa.

Majaliwa hakuweza kushiriki Mkitano Mikuu miwili ya CCM kutokana na ziara za kikazi

Akiongea mnamo Julai 26, 2025, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kupiga kura.

Mabadiliko haya yanakuwa nyongeza ya mabadiliko ya mfumo wa uteuzi wagombea wa CCM wa nafasi za dola yaliyofanywa katika mkutano mkuu wa mwezi Mei, 2025 uliofanyika jijini Dodoma.

Hatua hii inaifanya CCM kuweka rekodi kwa kufanya Mkutano Mkuu wake mara tatu katika mwaka wa uchaguzi katika historia nzima ya uwepo wake.