
Mahakama Kuu Yaridhia Mashahidi wa Siri Kesi Nyingine ya Tundu Lissu
Katika uamuzi wake Jaji Elizabeth Mkwizu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam amesema kuwa maombi hayo hayakuwa na mashiko akibainisha kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ulizingatia haki ya pande zote ikiwemo mshtakiwa kusikilizwa kwa usawa na usalama wa mashahidi.







