Mwanasheria Mkuu Ampeleka Mwabukusi Kamati Ya Maadili. Ni Wakili Anayesimamia Kesi ya Kupinga Mkataba wa Bandari
Mwabukusi anatakiwa kupeleka utetezi wake katika Kamati ya Maadili ya Mawakili ndani ya siku ishirini na moja. Kama utetezi wake hautakubalika moja ya adhabu inayotegemewa katika shauri hili ni kuvuliwa uwakili kwa kuondolewa katika orodha ya mawakili Tanzania.