The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Nini Hupelekea Mabadiliko ya Tabianchi?

Joto likiongezeka hubadilisha viashiria vingine vya hali ya hewa na tabianchi ya eneo kama vile mvua, joto la eneo, upepo nakadhalika.

subscribe to our newsletter!

Maelezo yanayofuata yametolewa kutoka sauti kwenda kwenye maneno kutoka kwenye mahojiano maalum ambayo The Chanzo imefanya na Dk Baruani Mshale, mtaalamu wa masuala ya maliasili na mabadiliko ya tabianchi. Uhariri umefanyika kuboresha usomaji.

Mabadiliko ya tabianchi yanasababishwa na ongezeko la gesi ambazo ziko kwenye anga letu, ambazo hizi gezi zinaitwa greenhouse gases. Nakosa Kiswahili chake hapo. Lakini hizi greenhouse gases ni gesi ambazo zipo katika anga letu na zenyewe kazi yake ni-.

Labda nirudi nyuma kidogo. Maisha hapa duniani yanawezekana kutokana na hali iliyopo hapa. Hali kwa maana ya kwamba hewa iliyopo, maji, na mazingira mengine. Na tunahitaji, viumbe vilivyopo, vinahitaji joto la kiasi fulani.

Chanzo kikubwa cha joto ni jua. Mionzi ya jua inapiga kwenye uso wa dunia. Kuna ambayo inakuwa inaingia, inafyonzwa, ndani ya uso wa dunia, na kuna ambayo inaakisiwa na kurudi kwenye anga.

Ile inayorudi kwenye anga, kuna ambayo inazuiwa tena kuondoka na hizi zinazoitwa greenhouse gases, yaani hizo gesi ambazo ziko kwenye anga letu, zinazuia kiasi cha joto ambacho kingeweza kuondoka na kupotea tu kwenye anga.

SOMA ZAIDI: Mabadiliko ya Tabianchi Ni Nini? Mtaalam Afafanua

Kwa hiyo, kuwepo kwa hiyo layer, kama utandu fulani hivi, kama blanketi, ambayo imezunguka uso wa dunia, blanketi ya hizo gesi, ndiyo inayowezesha kwamba duniani, kwenye uso wa dunia, tunakuwa na kiwango fulani cha joto ambacho kinawezesha maisha yetu, pamoja na viumbe wengine, kuweza kustahimili na kuweza kuwepo hapa duniani.

Sasa, hizi gesi zikiongezeka ina maana zitazuia joto jingi zaidi kubaki katika uso wa dunia, joto ambalo lingeweza kuondoka baada ya kuakisiwa na uso wa dunia, [na] tukisema uso wa dunia tunamaanisha maeneo ambayo labda kuna maji, kwa mfano mito, bahari, maziwa, maeneo ambayo yamejengwa, maeneo ambayo hayajajengwa, ni misitu, maeneo ambayo yana jangwa, kunakuwa na mawe na udongo, mchanga, nakadhalika.Kila kimoja wapo kati ya hivi kina uwezo tofauti wa kuweza kusharabu na kuakisi ile mionzi ya jua ambayo inaondoka na kurudi angani. Kwa hiyo, sasa zile gesi, ambazo zipo kwenye anga letu, ndiyo zinazuia kiasi cha lile joto lisiondoke lote.

SOMA ZAIDI: Wananchi Mkuranga Walia Na Athari Za Mabadiliko Tabia Nchi

Hizi gesi zikipungua ina maana kiasi cha joto kinachoweza kuondoka kitaongezeka. Hizi gesi zikiongezeka ina maana zitazuia kiwango kikubwa zaidi cha ile mionzi pamoja na joto lake kubakia katika uso wa dunia.

Joto likiongezeka, kwa sababu zile gesi zimeongezeka na zinazuia lile joto jingi kuondoka, ina maana sasa uso wa dunia utakuwa na joto zaidi. Uso wa dunia ukiwa na joto zaidi, joto likiongezeka, kuna athari nyingine zitakazotokea, itapelekea mabadiliko katika hali ya hewa, pamoja na tabianchi.

Kwa sababu, kwa mfano, tukiangalia mzunguko wa mvua tunajua kabisa kwamba ule mvukizo unaotokea katika maji — iwe ni bahari, iwe ni mito na nini – halafu vikienda angani, ikaganda, halafu ndiyo mvua inakuja inanyesha, ina maana kama jua likiongezeka na joto likiongezeka, ule mvukizo, – evaporation, – itaongezeka, halafu baadaye mvua zitanyesha nyingi zaidi.

Kwa hiyo, nini kimepelekea haya mabadiliko ya tabianchi? Kilichopelekea haya mabadiliko ya tabianchi ni ongezeko la hizi gesi ambazo zinazuia mionzi, ile ya jua, ambayo inazuia joto, inakuwa na joto, sasa inazuiwa kuondoka, inabaki. Ikibaki, inaongeza joto.

SOMA ZAIDI: Ni Upi Mtazamo wa Wakulima Wadogo Juu ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi?

Joto likiongezeka linaenda kubadilisha pia viashiria vingine vya hali ya hewa na tabianchi ya eneo kama vile mvua, joto la eneo, upepo nakadhalika, vyote vinaenda vikibadilika.

Lakini kilichoanzisha yale mabadiliko ni kuongezeka kwa joto, ndiyo ile dhana inayoitwa global warming. Kwamba pametokea hiyo global warming, joto limeongezeka, dunia imepata joto zaidi, na tabianchi ya eneo inaenda ikibadilika. Kwa hiyo, hiyo ndiyo kinachopelekea kutokea kwa mabadiliko ya tabianchi.

Kwa nini sasa?

Na kwa nini tunazungumzia mabadiliko ya tabia nchi sasa? Ongezeko la hizi gesi, kama nilivyosema, limetokea zaidi katika miaka 100 mpaka 150 iliyopita. Na hiki ndicho kipindi ambacho tumeshuhudia maendeleo ya kasi zaidi katika jamii mbalimbali za binadamu duniani.

SOMA ZAIDI: Mabadiliko ya Tabianchi Yatajwa Kuathiri Kilimo cha Korosho Lindi, Mtwara

Hapa ndipo kipindi ambako kumekuwa na uvumbuzi wa viwanda. Mbinu nyingine za njia tofauti tofauti za usafirishaji. Tumeongezeka idadi ya binadamu ambao tupo duniani, sasa hivi tunakaribia sijui bilioni nane. Viwanda vimeongezeka vimekuwa vingi.

Kwa hiyo, ukiangalia kuanzia mwaka 1600 mpaka sasa, ukitengeneza grafu, utaona kabisa joto la dunia lilikuwa kiasi fulani, lakini katika miaka 100 mpaka 150 iliyopita, imeenda ikiongezeka kwa kasi kubwa sana.

Na ndiyo kipindi ambacho tumekuwa na maendeleo mengi sana ya viwanda. Ina maana viwanda vyetu vimezalisha hizi gesi, hasa gesi ya hewa ukaa, kwenda kwenye anga na kusababisha mabadiliko ya tabianchi.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *