The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Uchambuzi wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Kwa Mwaka 2024/25

Katika mwaka huu wa fedha bajeti ya Wizara ya Elimu imechukua asilimia 3.99 ya bajeti yote ya Serikali.

subscribe to our newsletter!

Bunge la Tanzania siku ya Mei 7, 2024 lilijadili na kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2024/25 ambapo jumla ya shilingi trilioni 1.97 zimepanga kutumika na Wizara hiyo. Kiwango hiki ni sawa na ongezeko la asilimia 17.2 ukilinganisha na bajeti ya wizara hii ya mwaka 2023/24.

Katika mwaka huu wa fedha bajeti ya Wizara ya Elimu imechukua asilimia 3.99 ya bajeti yote ya Serikali. Hii inapelekea kuwa bajeti ya sekta ya elimu kwa mwaka 2024/25 kufikia asilimia 14 ya bajeti nzima ya Serikali, hii ni baada ya kujumlisha na matumizi ya bajeti ya TAMISEMI kwenye elimu.

SOMA ZAIDI: Uchambuzi Bajeti ya TAMISEMI 2024/25

Uchambuzi wetu, unatoa alama katika vipengele mbalimbali vya bajeti kwa madaraja matatu A ikionesha inaridhisha, B inaridhisha ingawa ina changamoto na C ina changamoto  za msingi.

Sehemu ya kwanza tuliyoangalia ni eneo la upelekaji fedha iliyotengwa kwenye bajeti. Katika eneo hili, tumeipatia Wizara ya elimu alama A. Hii inatokana na ukweli kwamba katika kuanzia mwaka wa fedha 2020/21 hadi 2022/23 Wizara hii imekuwa kipokea fedha kwa zaidi ya asilimia 100 ya bajeti iliyotengwa.  Na kwa mwaka wa fedha 2023/24 hadi kufikia Aprili 15, 2024 Wizara ilipokea asilimia 83 ya bajeti.

Eeneo la pili tuliloliangalia ni eneo la mikopo ya elimu ya juu. Kwa mwaka wa fedha 2024/25 mikopo ya elimu ya juu inachukua asilimia 60 ya bajeti ya maendeleo, ambapo Wizara imepanga kuongeza idadi ya wanufaika kutoka 223,201 mwaka 2023/24 ambapo Serikali ilitenga shilingi bilioni 786 hadi wanufaika 252,245 mwaka 2024/25 ambapo Serikali imepanga kutumia shilingi bilioni 801 kwenye eneo hili.

SOMA ZAIDI: Uchambuzi: Bajeti ya Wizara Ya Nishati 2024/25 Ni Ndogo Zaidi Kutokea Katika Kipindi Cha Miaka Mitano. Hiki Ndicho Kilichosababisha

Kwenye eneo hili tumeipa Wizara alama A kwa sababu kiwango hiki kikubwa cha fedha kilichotengwa kimepelekea ongezeko la upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa zaidi ya asilimia 90 ya waombaji wa mikopo hiyo. Sambamba na hilo Serikali ilianza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa ngazi stashahada kwa mara ya kwanza ambapo wanafunzi 2,299 walipewa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 6.11.

Pamoja na manufaa ya kutengwa kwa pesa nyingi kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, tumeona kwamba mikopo hii inachukua sehemu kubwa ya bajeti ya maendeleo jambo ambalo linahatarisha maendeleo ya ujumla katika eneo la elimu ya juu, sayansi na teknolojia kwa ujumla.

Eneo la tatu tuliloliangalia ni muundo wa taarifa ya bajeti, kwa mwaka huu eneo hili tunalipa alama C. Hii inatokana na ukweli kwamba taarifa ya bajeti haijaweza kueleza bayana kiwango cha fedha kilichotengwa kwenye maeneo ya vipaumbele, kwa mfano suala la utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu ambao umeanza mwaka huu.

SOMA ZAIDI: Uchambuzi: Bajeti ya Wizara ya Kilimo 2024/25 Inaakisi Umuhimu wa Sekta ya Kilimo?

Maeneo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, sayansi na teknolojia, utafiti na masuala ya uboreshaji ubora wa elimu imeelezwa mikakati tu pasipo kuanisha kiwango cha fedha ambacho Serikali inategemea kutumia katika kipindi husika.

Eneo la nne tuliloangalia ni utoaji wa taarifa za utekelezaji wa bajeti iliyopita, eneo hili tumetoa alama B, kwa kuwa sehemu kubwa bajeti imeweza kutoa mrejesho wa kutosha kuhusu vipaumbele vya bajeti 2023/24.

Hii ikiwa ni pamoja na namna Serikali ilivyotelekeza masuala kama Sera ya  Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu, uwezeshaji wa wataalamu, ujenzi wa miundombinu na uwezeshaji wa ubunifu na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia. 

Sababu ya kuipa alama B eneo hili ni kutokana na taarifa ya Serikali kushindwa kuainisha kiwango cha fedha kilichotumika katika utekelezaji wa vipaumbele na masuala yaliyoainishwa. 

Mfano, Serikali imeeleza namna ilivyoweza kuendesha mafunzo kwa walimu na watendaji wake nchini ili kutekelezwa sera na mitaala mipya ya elimu, lakini katika taarifa hiyo haielezi ni kiwango gani cha fedha za bajeti kimetumika.

Digital Freedom and Innovation Day
The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on Saturday April 20, 2024 at Makumbusho ya Taifa.

Register to secure your spot

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *