The Chanzo is hosting Digital Freedom and Innovation Day on April 20, 2024. Register Here

Search
Close this search box.

Author: Lukelo Francis

Wanasiasa, Wanaharakati Wataka Masheha Wapigiwe Kura Zanzibar

Kumekuwapo na tuhuma kwamba katika utekelezaji wa majukumu yao Masheha wamekuwa wakikipendelea chama cha CCM na wakila njama za kuvidumaza vyama vya upinzani. Tuhuma hizi huibuka zaidi wakati wa michakato ya chaguzi kuu kuanzia utoaji wa kadi za Mzanzibari Mkaazi na usajili wa daftari la wapiga kura.

Wachumi: Tutegemee Bei za Bidhaa, Huduma Kushuka 2022

Wachumi hao wanabainisha juhudi zinazoendelea kuchukuliwa duniani za kupambana na janga la UVIKO-19, ikiwemo matumizi ya chanjo; kukamilika kwa ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali; pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha kama zitaendelea kama msingi wa matumaini yao hayo.

Mpango wa Wasanii Kulipwa Mirabaha Umefikia Wapi?

Mpango huo ulitegemewa kuanza Disemba 2021, lakini wakati Januari 2022 nayo inaenda kuisha wasanii wanasema kwamba hawajaanza kupokea mirabaha hiyo, huku wengi wakibainisha kwamba hawajui hata mchakato wenyewe umekwamia wapi.

Kilichojificha Nyuma ya Kuvuja kwa Video za Utupu Mitandaoni

Kwa mujibu wa wahanga, video nyingi za utupu zinazosambaa mitandaoni zimevujishwa na kikundi cha wahalifu walioamua kuchukua hatua hiyo baada ya mabinti husika kukataa kutoa fedha ambazo wahalifu hao wamekuwa wakiwaomba ili wasivujishe video hizo za kashfa.