Wabunge Wataka Sheria, Kanuni Kandamizi za Uandishi wa Habari Kurekebishwa
Watunga sheria hao walitoa wito huo wakati wakiongea na The Chanzo pembezoni mwa mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa-Tan) yaliyofanyika mnamo Februari 12, 2022, yaliyolenga kuwafahamisha wawakilishi hao wa wananchi kwenye vifungu vya sheria na kanuni vinavyominya uhuru wa vyombo vya habari nchini.